Wachezaji wetu watatu waliokuwa kwenye majukumu ya timu za Taifa watatua nchini leo na kujiunga moja kwa moja na wenzao kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy.
Nyota hao ni kiungo Rally Bwalya aliyekuwa na kikosi cha Timu ya Taifa ya Zambia, Taddeo Lwanga aliyekuwa Uganda na Medie Kagere aliyekuwa na kikosi cha Rwanda.
Baada ya kufika nchini wachezaji hao wanatarajia kuanza mazoezi kesho pamoja na wenzao kujiandaa na mtanange huo.
Advertisement
Nyota wengine watatu Peter Banda, Duncan Nyoni waliokuwa na kikosi cha Malawi pamoja na Joash Onyango aliyekuwa Kenya wanatarajia kurejea nchini kesho.
Mchezo wetu dhidi ya Jwaneng Galaxy utapigwa Jumapili Oktoba, 17 nchini Botswana.