Simba Sports Club
News

Bwalya: Hayakuwa maamuzi rahisi kuondoka Simba

18 Jun 2022

Bwalya amesema Simba ni chapa kubwa (brand) barani Afrika na imemfanya kutambulika kirahisi kila mahali anapokwenda hivyo daima itabaki moyoni kwake.

Bwalya ameongeza kuwa ameshinda mataji yote ya ndani akiwa ya kikosi chetu pamoja na kufanya vizuri katika Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu uliopita na hilo ni jambo la kujivunia kwake.

"Nitawakumbuka wachezaji wenzangu, benchi la ufundi, viongozi na mashabiki kwa ushirikiano mkubwa walionipatia, hali ya hewa ya Dar es Salaam na chakula katika kipindi chote cha miaka miwili nilichokuwa hapa.

Advertisement

"Ni ngumu kusema kwa heri kwa klabu ambayo naichukulia kama familia kwangu. Nimeishi vizuri hapa na nimepata ushirikiano mkubwa kutoka kila pande iliyonizunguka lakini haya ni maisha, muda wa kutafuta changamoto mpya umefika," amesema Bwalya.

Bwalya amesema atawakumbuka wachezaji wote pamoja na benchi la ufundi lakini Chris Mugalu atamkumbuka zaidi kwa kuwa walikuja siku moja na kuishi chumba kimoja.

"Kama nilivyosema Simba ni familia yangu, tumeishi vizuri na nitawakumbuka sana wachezaji wenzangu lakini Mugalu itakuwa zaidi sababu tulisaini mkataba wa kujiunga hapa siku moja na tunaishi nyumba moja ni marafiki wakubwa," amesema Bwalya.

Back to homepage
Share this story