Utaratibu wa bodi kukutana mara kwa mara ni kawaida kwa taasisi kwa ajili ya kujadili masuala ya kiuendeshaji na mambo mbalimbali.
Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni kuhakikisha tunafikia malengo tuliyojiwekea ya kufika Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, kutetea ubingwa wa ligi kuu pamoja na Azam Sports Federation Cup.
Advertisement
Aidha, kuhakikisha Simba Queens inatetea taji lake la Serengeti Lite Women's Premier League ambapo hadi sasa ligi ikiwa imesimama imeshinda mechi zote 11 za mzunguko wa kwanza.