Simba Sports Club
News

Bodi ya Ligi yaahirisha mchezo dhidi ya Dodoma Jiji

12 Feb 2025

Sababu ya kuahirishwa mchezo huo ni kutokana na wachezaji wa Dodoma Jiji kupata ajali katika Wilaya ya Ruangwa wikiendi iliyopita.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi inasema Maafisa na baadhi ya wachezaji hawapo sawa kiafya hivyo hawataweza kuwa sehemu ya mchezo hivyo mechi imeahirishwa.

Advertisement

TPLB imesema itatoa taarifa muda si mrefu ya lini mchezo huo utapigwa tena.

Back to homepage
Share this story