Simba Sports Club
News

Bocco: Tunawashukuru mashabiki wetu kwa sapoti kubwa

30 Apr 2023

Bocco amesema mashabiki wetu wamekuwa pamoja na timu katika nyakati zote bila kujali matokeo gani yamepatikana.

"Kwa niaba ya wachezaji nawashukuru mashabiki wetu kwakuwa nasi siku zote katika mazingira yote. Iwe furaha au huzuni wapo pamoja nasi."

"Tumetoka kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika lakini wamekuja kwa wingi Uwanja wa Ndege kuja kutupokea, tuna uthamini mchango wao na tumejipanga kuwalipa furaha wakati mwingine," amesema Bocco.

Advertisement

Akizungumzia michuano ya Ligi ya Mabingwa, Bocco amesema tunaendelea kujifunza kila wakati ili wakati mwingine tufanye vizuri zaidi.

"Miaka ya nyuma ilikuwa tukifikia hatua ya makundi ni mafanikio, sasa tunaweza kufika robo fainali bila wasi wasi, tunaamini tutaweza kufika mbali zaidi kipindi kijacho," amesema Bocco.

Back to homepage
Share this story