Nyota watatu wakiwamo Nahodha John Bocco, Bernard Morrison na Taddeo Lwanga wameingia fainali ya kumtafuta mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Mei (Emirate Aluminium Profile Simba Fans Player of the Month).
Kabla ya kuingia fainali wachezaji walioingia tano bora ni pamoja na Pascal Wawa na Mohamed Hussein lakini Kamati Maalumu imewachuja na kubaki na nyota hao watatu.
Advertisement
Bocco, Morrison na Lwanga watapigiwa kura na washabiki wetu kupitia tovuti hii rasmi ya klabu na atakayepata kura nyingi atatangazwa mshindi.
Tuzo hii inadhaminiwa na Kampuni ya Emirate Aluminium Profile na ilianza kutolewa Februari mwaka huu ambapo hutoa kitita cha Sh 1,000,000 kwa mshindi.
[totalpoll id="4384"]