Bocco ameyasema hayo wakati kikosi kikifanya mazoezi ya utimamu wa mwili katika Uwanja wa Kirumba kujiandaa na mchezo wa Jumapili baada ya kuwasili asubuhi.
Bocco amesema tunajua mchezo utakuwa mgumu na tunaiheshimu Geita lakini tunaamini maandalizi yetu tuliyofanya yatatuwezesha kuondoka na alama zote tatu ugenini.
Advertisement
"Maandalizi yanaendelea vizuri, tupo kwenye hali nzuri tunaamini mchezo utakuwa mgumu tunaiheshimu Geita lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.
"Siku zote mechi za mikoani zinakuwa ngumu na tunajua tupo mzunguko wa pili hatupaswi kudondosha alama kwakuwa malengo yetu ni kuchukua ubingwa," amesema Bocco.