Simba Sports Club
News

Bocco kuongoza mashambulizi dhidi ya Jwaneng Galaxy

17 Oct 2021 By simbasc 1,008 views

Nahodha John Bocco ataongoza mashambulizi dhidi ya Jwaneng Galaxy katika mchezo wa hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa Uwanja wa Taifa wa Botswana saa 10 jioni.

Bocco atapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Bernard Morrison, Hassan Dilunga na Rally Bwalya.

Mlinzi wa kati Henock Inonga amepangwa kusimama na Pascal Wawa huku kiungo Sadio Kanoute aliyekuwa majeruhi akirejea moja kwa moja kikosini.

Kikosi Kamili kilivyopangwa.

Advertisement

Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Pascal Wawa (6), Henock Inonga (29), Taddeo Lwanga (4) Bernard Morrison (8) Sadio Kanoute (13), John Bocco (22), Rally Bwalya (8), Hassan Dilunga (24).

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Peter Banda (11), Erasto Nyoni (18), Duncan Nyoni (23), Mzamiru Yasin (19),
Israel Patrick (5), Joash Onyango (16), Medie Kagere (14), Kennedy Juma (26).

Back to homepage
Share this story