Simba Sports Club
News

Bocco arejea na 'Hat trick' dhidi ya Ruvu

19 Nov 2022

Bocco alitupatia bao la kwanza dakika ya tatu baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na mlinzi Mohamed Hussein.

Dakika ya 17 Bocco alitupatia bao la pili baada ya kumalizia pasi ya Clatous Chama kufuatia shambulizi lililoanzia kwa mlinzi wa kulia Shomari Kapombe.

Kapombe alitupatia bao la tatu dakika ya 36 baada ya kumzidi ujanja mlinzi mmoja wa Ruvu akimalizia pasi safi kutoka kwa Chama.

Advertisement

Kiungo mkabaji Sadio Kanoute alishindwa kuendelea na mchezo na kutolewa dakika ya 37 baada ya kuumizwa nafasi yake ikachukuliwa na Victor Akpan.

Bocco alitupatia bao la nne na kukamilisha hat trick yake dakika ya 70 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Mzamiru Yassin.

Kocha Juma Mgunda aliwatoa Henock Inonga, Bocco, Joash Onyango na Mzamiru na kuwaingiza Mohamed Ouattara, Kennedy Juma, Kibu Denis na Nassor Kapama.

Back to homepage
Share this story