Baada ya kupona majeraha Bocco amerejesha makali yake ambapo amefunga mabao matatu katika mechi tatu mfululizo ikiwemo dhidi ya Azam FC jana.
Bocco amesema siku zote mashabiki wanakusifu unapofanya vizuri na ukifanya vibaya wanakukosoa hivyo kama mchezaji lazima kupambana kupita nyakati zote.
Advertisement
"Nilipitia kipindi kigumu wakati tunaanza msimu kutokana na majeruhi. Siku zote mashabiki watakusifu ukifanya vizuri na watakukimbia ukifanya vibaya unapaswa kupitia nyakati zote.
"Nimejipanga kuhakikisha ninafanya vizuri katika mechi zilizobaki ili kumaliza msimu vizuri," amesema Bocco.