Stars itacheza na The Cranes Jumamosi jijini Kampala ikiwa nyuma kwa bao moja baada ya kufungwa katika mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi iliyopita.
Bocco amejiunga na kikosi hapa Sudan Jumamosi iliyopita lakini baada ya kuitwa Stars imebidi aondoke usiku wa kuamkia leo kwa ajili ya majukumu ya Timu ya Taifa.
Advertisement
Juzi Kocha msaidizi Seleman Matola jana aliweka wazi kuwa Bocco na Sadio Kanoute ambao walichelewa kujiunga na timu watakuwa sehemu ya kikosi kitakachoshuka dimbani leo kuikabili Al Hilal.