Simba Sports Club
News

Biriani la Derby laliwa Temeke

3 Nov 2023

Biriani la leo ni maalum kabisa kwa ajili ya mchezo wetu wa Jumapili dhidi ya Yanga ambao tumejipanga kikamilifu kuhakikisha tunashinda.

Hamasa hiyo imeanzia Uwanja wa Benjamin Mkapa nakuzunguka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Temeke.

Advertisement

Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally amesema mchezo wa Derby umebeba taswira ya soka Tanzania hivyo mashabiki wanapaswa kujitokeza kwa wingi uwanjani kuisaidia timu kupata ushindi ambao utawapa furaha.

"Mchezo wa Derby ya Kariakoo ndio kioo cha soka la Tanzania, furaha ya ushindi wake inadumu kuliko mechi yoyote hivyo Wanasimba kateni tiketi tukutaje Jumapili Benjamin Mkapa kuisaidia timu yetu kupata ushindi," amesema Ahmed.

Back to homepage
Share this story