Simba Sports Club
News

Betway ndiye Mdhamini wetu Mkuu

29 Jul 2025

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu, Salim Abdallah 'Try Again' amesema malengo yetu kwa sasa ni kuhakikisha brand yetu inaendelea kukua siku hadi siku ndani na nje ya Afrika.

"Ndani ya Bodi ya Simba kazi yetu ni kuhakikisha brand yetu inazidi kukua siku hadi siku. Nguvu kubwa ya Simba ni mashabiki wake ambao wanafanya wadhamini kama Betway waje kuwekeza. Tunataka Simba iwe na nguvu ndani na nje ya Afrika," amesema Try Again.

Kwa upande wake Mkuu wa Udhamini wa Betway Afrika, Jason Shield ameweka wazi kuwa kilichowavutia kuwekeza katika klabu yetu ni umaarufu mkubwa ndani ya Afrika huku akisema walitufuatilia kwa miaka sita.

"Tumeingia Simba sababu ni timu kubwa Afrika, ni timu ambayo inajulikana pande zote za bara la Afrika na hilo ndilo tunaangalia zaidi kwenye biashara. Tulikuwa tunafuatilia kwa miaka sita lakini sasa imekuwa kweli. Tunafuraha kufanikisha jambo hili," amesema bwana Jason.

Advertisement

Nae Mtendaji Mkuu wa Klabu, Zubeda Sakuru amesema mkataba tulioingia na Betway unaekwenda kuleta mapinduzi makubwa ya soka ndani ya Tanzania na pia utatuongezea nguvu nakuwa klabu namba moja Afrika.

"Udhamini huu ambao thamani yake ni bilioni 20 kwa miaka mitatu unaonyesha Simba tumedhamiria kuleta mabadiliko yakuwa klabu kubwa ndani ya Afrika," amesema CEO, Zubeda.

Makamu wa kwanza wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania, Athumani Nyamlani ametupongeza kwa kuingia mkataba huu na Betway huku akisisitiza kila pande kuhakikisha anafuata matakwa ya mkataba ili kuepuka migongano.

"Nitoe pongezi kwa Simba, ni tukio ambalo kila siku TFF tunaliimba, ni hatua kubwa sisi TFF tunasisitiza kila upande utilize wajibu wake," amesema Nyamlani.

Back to homepage
Share this story