Simba Sports Club
News

Beno: Najisikia faraja kila nifika Mbeya

16 Jan 2022

Mlinda mlango namba mbili, Beno Kakolanya ameweka wazi kuwa anajisikia furaha anapokanyaga jijini Mbeya kwa ajili ya kucheza mechi.

Beno ambaye ni mzaliwa wa Mbeya amesema historia yake ya soka ilianzia jijini humo hivyo kila akifika anakuwa na kumbukumbu nyingi.

Pamoja na maambo mengine nyanda huyo ameuzungumzia mchezo wetu wa kesho dhidi ya Mbeya City kuwa utakuwa mgumu lakini anaamini tutaibuka na ushindi kutokana na ubora wa kikosi chetu pamoja na maandalizi tuliyofanya.

Advertisement

"Ninasikia furaha sana kila ninapofika hapa. Kumbukumbu zangu zote za soka zilianzia hapa. Kila nikija kitu cha kwanza kinachonijia kichwani ni mama yangu.

"Ingawa kwa sasa hayupo lakini mama alikuwa ananipa moyo na amechangia pakubwa mimi kufika hapa. Kwa kifupi huwa nafurahi sana kucheza katika ardhi ya nyumbani," amesema Beno.

Back to homepage
Share this story