Simba Sports Club
News

Benchikha: Tunahitaji kushinda kesho bila kuangalia matokeo ya wengine

1 Mar 2024

Benchikha amesema tunahitaji kushinda kwa ajili ya mashabiki wetu ambao wamekuwa nasi katika kipindi chote na wanastahili kupata furaha.

Akizungumzia mchezo wenyewe Benchikha amesema Galaxy wamebadilika na kikosi chao kinaimarika siku hadi siku kwahiyo tutaingia kwa tahadhari lengo likiwa ni kuhakikisha tunashinda.

"Sisi tunatakiwa kushinda hatumuangalii mtu wala matokeo ya timu nyingine, hii ndio faida yetu, tunatakiwa kuwa imara tushinde kwa ajili ya Mlmashabiki wetu na Watanzania wote wanaotusapoti.

Advertisement

"Itakuwa mechi ngumu sana naona Galaxy wana muendelezo mzuri katika mechi na mechi.Galaxy tuliocheza nao Botswana sio hii imebadilika wanacheza vizuri lakini tumejipanga," amesema Benchikha.

Kwa upande mshambuliaji Pa Omar Jobe amesema hakuna kitu kingine kinahitajika zaidi ya ushindi na kuisaidia timu kufuzu hatua ya robo fainali.

"Lengo letu ni kushinda, hii ni mechi ya mwisho kwetu tuna faida ya kucheza nyumbani, tunaenda kwa Lengo moja la kutafuta ushindi," amesema Jobe.

Back to homepage
Share this story