Simba Sports Club
News Videos

Benchikha: Mechi dhidi ya Wydad ni ya maamuzi kwetu

18 Dec 2023

Benchikha amesema tunahitaji kupata pointi tatu kwenye mchezo huo ambao tunaamini utakuwa mgumu kutokana na ubora walionao.

Hata hivyo Benchikha amesema anawaamini wachezaji wake na wapo kwenye hali nzuri kuhakikisha tunapata ushindi na kucheza soka safi.

"Kwetu ni mechi ya maamuzi. Tupo kamili kuhakikisha tunapata ushindi na kucheza soka safi, nawaamini wachezaji wangu wapo tayari kuhakisha ushindi unapatikana," amesema Benchikha.

Advertisement

Kwa upande wake nahodha msaidizi, Mohamed Hussein 'Zimbwe Jr' amesema mchezo wa kesho ni fainali kwetu ambao tunahitaji kushinda kwa kila namna ili kurejesha matumaini ya kufuzu hatua ya robo fainali.

Zimbwe Jr ameongeza kuwa kila mchezaji yupo tayari kwa ajili mchezo huo na atapambana kuhakikisha Wanasimba wanapata furaha kwa kupata ushindi.

"Ni fainali kwetu, tunahitaji ushindi ili kufufua matumaini ya kufanya vizuri, sisi kama wachezaji tupo tayari kupambana hadi mwisho ili kupata ushindi," amesema Zimbwe Jr.

Back to homepage
Share this story