Simba Sports Club
News

Benchikha awamwagia sifa wachezaji ushindi dhidi ya Singida FG

3 Jan 2024

Benchikha amesema tulicheza vizuri kuanzia kwenye kuzuia hadi kushambulia na kuweza kumiliki sehemu kubwa ya mchezo.

Hata hivyo Benchikha ameisifu Singida Fountain Gate kwa kucheza soka la kasi pamoja na mashambulizi haraka ingawa tuliweza kuwamudu.

Advertisement

"Nawapongeza wachezaji wangu, tumecheza vizuri. Ilikuwa mechi ngumu yenye kasi lakini tulikuwa bora ndio maana tumeshinda."

"Singida ni timu nzuri na inacheza soka la kushambulia na ilitupa upinzani mkubwa ingawa tulikuwa bora zaidi yao," amesema Benchikha.

Back to homepage
Share this story