Simba Sports Club
News

Benchikha arejea, aongoza mazoezi ya mwisho

14 Mar 2024

Benchikha alikwenda nchini Algeria kwa ajili ya kushiriki kozi fupi ya ukocha na tayari amerejea na kesho atakuwa kwenye benchi kukiongoza kikosi dhidi ya Mashujaa kwenye mchezo utakaopigwa Uwanja wa Azam Complex saa 2:15 usiku.

Katika mazoezi hayo yaliyofanyika jioni katika Uwanja wetu wa Mo Simba Arena wachezaji wote wameshiriki kikamilifu na wapo kwenye hali nzuri.

Advertisement

Tutaingia kwenye mchezo wa kesho tukiwa na kumbukumbu nzuri ya ushindi wa mabao 3-1 tuliopata juzi dhidi ya Singida Fountain Gate.

Back to homepage
Share this story