Katika mazungumzo hayo Benchika amewakumbusha wachezaji majukumu yao na kuhakikisha wanajituma ili kuwapa furaha mashabiki.
Benchikha amewaambia wachezaji anawaamini na kwa pamoja tunaweza kubadili hali ya hewa iliyopo sasa na kurudisha furaha na kuanza kupata ushindi.
Kocha Benchikha ameongezeka kuwa yupo tayari kufanya kazi na mchezaji yoyote anayejituma huku akiweka wazi hatovumilia wazembe na wavivu.
Advertisement
"Nina furaha kuwa hapa nafurahi kuwa nyinyi, nipo hapa kwa ajili ya kushinda tukishirikiana kwa pamoja, kila mmoja atapata nafasi kikubwa kujituma uwanjani," amesema Benchikha.
Benchikha tayari amekutana na Bodi ya Wakurugenzi na kuongea na Waandishi wa Habari kuhusu mipango yake ya timu na leo ndio amekutana na wachezaji.