Simba Sports Club
News

Basigi: Hatutakiwi kuangusha hata alama moja Mzunguko wa pili

21 Jan 2025

Basigi ameyasema hayo wakati akizungumzia maandalizi ya mchezo wa kesho dhidi ya Mlandizi Queens utakaopigwa saa nane mchana katika Uwanja wa KMC Complex.

Basigi amesema ingawa tunaongoza tukiwa juu kwa alama mbili dhidi ya JKT Queens wanaotufuata lakini hatuna uhakika wa asilimia 100 ya kutwaa ubingwa hivyo tunatakiwa kushinda mechi zote.

Advertisement

Akizungumzia mchezo dhidi Mlandizi, Basigi amesema utakuwa mgumu lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda.

"Sio mechi tu ya Mlandizi bali mzunguko wa pili wa ligi utakuwa mgumu hasa ukiangalia tumepishana alama chache hivyo tunatakiwa kushinda mechi zote tisa ikiwemo ya kesho," amesema Basigi.

Back to homepage
Share this story