Simba Sports Club
News

Barker: Tunahitaji kuwa na muendelezo chanya

13 Mar 2026

Barker ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya TRA United utakaopigwa katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid saa 10 jioni.

Akizungumzia hali ya kikosi Barker amesema wachezaji wapo kwenye hali nzuri isipokuwa tutaendelea kumkosa mshambuliaji, Seleman Mwalimu ambaye anaitumikia adhabu.

"Kikosi chetu kinazidi kuimarika na tunahitaji kuendelea kupata ushindi kwenye mechi zetu ili kujiweka kwenye nafasi nzuri, kuhusu mchezo dhidi ya TRA United kesho tupo tayari na hatuna majeruhi," amesema kocha Barker.

Advertisement

Kwa upande wake mlinzi wa kulia, David Kameta 'Duchu' amesema pamoja na ugumu na upinzani ambao tutakutana nao lakini tumejipanga na malengo yetu ni kupata alama tatu.

"Kwa upande wetu kama wachezaji tupo tayari kwa mchezo, tunafahamu utakuwa mgumu na tunawaheshimu wapinzani wetu lakini tupo tayari kupambana hadi mwisho kupata alama tatu," amesema 'Duchu'.

Back to homepage
Share this story