Barker amesema tuna faida kubwa ya kucheza mbele ya mashabiki wetu na wachezaji wapo tayari ingawa tunakutana na mpizani mgumu.
Barker ameongoza kuwa ushindi dhidi ya ES Tunis ndio jambo pekee ambalo tumejipanga kulifanya kwakuwa malengo yetu ni kufuzu hatua inayofuata.
"Tunajua tuna faida nzuri ya kucheza mbele ya mashabiki wetu lakini tunapaswa kuwa makini na kujitoa kwa asilimi 100 ili kupata ushindi dhidi ya ES Tunis Kesho. Ninawaamini wachezaji wangu na wapo tayari," amesema Barker.
Akizungumza hali ya kikosi Barker amesema "tumeongeza ufanisi katika idara yetu ya ushambuliaji baada ya kusajili nyota wapya na tuna matumaini ya kufanya vizuri.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mshambuliaji, Morice Abraham amesema morali za wachezaji zipo juu na kila mmoja anajua umuhimu wa ushindi katika mchezo huo.
"Morali zipo juu na kila mchezaji anajua umuhimu wa ushindi kwenye mchezo wa kesho ndio maana hakuna maelekezo mengi, ushindi ndio kitu ambacho kipo vichwani mwetu," amesema Morice.