Barker amesema kwasasa tumerejesha nguvu kwenye michuano ya Ligi pamoja na CRDB Federation kwahiyo kila mchezo kwetu tunaupa umuhimu mkubwa ili kuweza kufikia malengo tuliyojiwekea.
Akizungumzia mchezo wa kesho, Barker amesema maandalizi ya mchezo yamekamilika na wachezaji wapo kwenye hali nzuri na morali zipo juu na wapo tayari kuipigania timu kupata ushindi.
Barker ameongeza kuwa malengo yetu ni kuhakikisha tunacheza soka safi pamoja na kupata ushindi ili kuwafurahisha mashabiki wetu.
"Maandalizi ya mchezo dhidi ya Prisons yamekamilika na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri, tunahitaji kushinda ili kuendelea kurudisha imani kwa mashabiki na pia kupigania ubingwa wa Ligi," amesema Barker.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kati, Vedastus Masinde amesema wapo tayari kufuata maelekezo watakayopewa na walimu ili kuhakikisha ushindi unapatikana.
"Kwa upande wetu wachezaji tumejiandaa vizuri na kila atakayepata nafasi kwenye mchezo wa kesho atakuwa tayari kuipigania timu kupata matokeo chanya," amesema Masinde.