Barker amesema mchezo utakuwa mgumu kutokana na kila timu kuhitaji alama tatu kwa sababu kila moja haipo nafasi nzuri kwenye msimamo ingawa tumejiandaa vizuri.
Akizungumzia hali ya kikosi, Barker amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na morali zipo juu na wapo tayari kuhakikisha malengo ya timu yanafikiwa.
"Utakuwa mchezo mgumu kwa timu zote mbili kutokana nafasi tulizopo haziridhishi, lakini sisi tumekuja na malengo ya kuhakikisha tunashinda ili kufufua matumaini ya kusonga mbele," amesema kocha Barker.
Kwa upande wake mlinzi wa kati, Rushine De Reuck amesema pamoja na kutoanza vizuri kwenye mechi zetu mbili za mwanzo wachezaji hawajakata tamaa na tupo tayari kupambana ili kupatikana kwa alama tatu.
"Bado tuna matumaini ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa kesho, tunafahamu itakuwa mechi ngumu na tunawaheshimu wapinzani wetu lakini tumekuja kushindana ili kupata matokeo mazuri," Rushine De Reuck, mlinzi wa kati.