Barker amesema anaendelea kukisuka kikosi imara na kuzidi kuwapa nafasi wachezaji wote waliopo ili kuwa na wigo mpana wa machaguzi.
Barker ameongeza kuwa tumeupa umuhimu mkubwa mchezo wa kesho na hatutaidharau Greenland na tutaingia uwanjani kwa kuchukua tahadhari zote.
Advertisement
"Tumeupa umuhimu mkubwa mchezo wa kesho tunahitaji kushinda ili kusonga mbele lakini nategemea kufanya mabadiliko kadhaa kwenye kikosi," amesema Barker.
Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Meja Isamuhyo jioni tayari kwa mchezo wa kesho.