Simba Sports Club
News

Barker: Kikosi changu kinazidi kuimarika

10 Feb 2026

Barker amesema wachezaji wanaonyesha jitihada kubwa ya kuhakikisha timu inarejea katika hali yake ya ushindi kwenye kila mchezo kitu ambacho kinampa matumaini makubwa.

Kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya KMC, Barker amesema utakuwa mgumu kutokana na mpizani wetu kutokuwa kwenye hali nzuri lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata matokeo chanya.

Barker ameongeza kuwa haitakuwa mechi rahisi licha ya KMC kuwa mkiani mwa msimamo ndio maana tumeweka nguvu kubwa kuhakikisha tunapata ushindi.

Advertisement

"Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wa kesho, wachezaji wapo kwenye hali nzuri na kikosi kinazidi kuimarika kila siku na matumaini ya kufanya vizuri ni makubwa," amesema Barker.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kulia David Kameta 'Duchu' amesema kila mmoja anafahamu umuhimu wa kushinda mchezo wa kesho pamoja na ugumu ambao tunategemea kukutana nao.

"Tunahitaji ushindi kwenye mchezo wa kesho dhidi ya KMC hatupo kwenye nafasi nzuri katika msimamo tunahitaji kushinda ili kurejesha matumaini," amesema Duchu.

Back to homepage
Share this story