Barker amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na wanafahamu ni mchezo muhimu kupata ushindi kwakuwa malengo yetu ni kushinda ubingwa wa michuano yote tunayoshiriki.
Barker amekiri kuwa tumekuwa tukitengeza nafasi nyingi kwenye mechi zetu lakini changamoto ikiwa ni kwenye kuzitumia kitu ambacho kinaendelea kufanyiwa kazi mazoezini.
"Malengo ya Simba kwenye kila mashindano inayoshiriki ni kutwaa ubingwa. Tumejipanga kukutana na upizani mkubwa kutoka kwa Dodoma Jiji lakini tumejipanga kuhakikisha tunashinda na kuvuka hatua hii," amesema Barker.
Akizungumza kuhusu hali ya majeruhi kikosini, Barker amesema "wachezaji wote wapo tayari kwa mchezo hata Elie Mpanzu ambaye amekosa mechi tatu zilizopita nae yupo kwenye mipango ya mechi ya kesho."
Kwa upande wake nahodha msaidizi, Rushine De Reuck amesema tutaingia kwenye mchezo wa kesho kuhakikisha tunacheza vizuri ili kuwafurahisha mashabiki wetu na kupata ushindi.
"Ili kuwa bingwa lazima ushinde mechi zote ambazo ni ngumu, na malengo yetu ni kutwaa ubingwa ingawa tunategemea tutapata ushindani mkubwa," amesema De Reuck.