Mtendaji Mkuu wa klabu, Barbara Gonzalez ameweka wazi kuwa lengo mama msimu huu ni kuhakikisha tunafika nusu fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Barbara amesema nguvu zilizokuwa zimewekwa kwa ajili ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika zimerudishwa Shirikisho suala ambalo hata kocha Pablo Franco ameambiwa.
Advertisement
Barbara ameongeza kuwa tunahitaji kufikia malengo ya msimu uliopita katika michuano ya Ligi ya Mabingwa na ikiwezekana tuyavuke ili kuendelea kuipeperusha vema bendera ya Tanzania Kimataifa.