Simba Sports Club
News

Barbara: Hakuna kulaumiana

21 Mar 2022

Mtendaji Mkuu wa klabu, Barbara Gonzalez amefunguka kuwa hatupaswi kulaumiana wala kunyoosheana vidole kwa matokeo ya jana badala yake kujipanga kwa mchezo wa mwisho unaofuata.

Barbara amesema bado tuna nafasi ya kutinga robo fainali kama tutashinda mchezo wetu wa nyumbani dhidi ya US Gendarmerie kwa hiyo hatupaswi kupoteza lengo.

Katika kuonesha umakini kuelekea mchezo huo Barbara amesema wachezaji wote wanatakiwa kurejea mazoezini Machi 27 kuanza rasmi kambi ya kuelekea mchezo huo.

Advertisement

"Yaliyopita si ndwele tugange yajayo, bado tuna nafasi ya kutinga robo fainali kama tutashinda mchezo wetu dhidi ya Gendarmerie. Kilichotokea jana ni sehemu ya mchezo wala hatupaswi kulaumiana.

"Wachezaji wote ambao watakuwa kwenye majukumu ya timu za taifa na wale watakaokuwa mapumziko watatakiwa kuripoti kambini haraka Ili tuanze maandalizi ya mchezo wetu wa mwisho mara moja," amesema Barbara.

Back to homepage
Share this story