Simba Sports Club
News

Bao la Sakho laingia tatu bora Afrika

20 Jul 2022 By simbasc 1,012 views
Bao la kiungo mshambuliaji Pape Sakho alilofunga katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya ASEC Mimosas limeingia tatu bora kwenye kinyang'anyiro ya kutafuta bao bora la mwaka. Sakho alifunga bao hilo Februari 13, katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa acrobatic akimalizia mpira wa krosi uliopigwa na mlinzi, Shomari Kapombe. Wachezaji ambao mabao yao yameingia tatu bora ni Gabadinho Mhango (Malawi & Orlando Pirates) Pape Ousmane Sakho (Senegal & Simba) Zouhair El Moutaraji (Morocco & Wydad Athletic Club) Tuzo za kutangaza bao bora ambazo mshindi atapatikana kwa kupigiwa kura nyingi zitafanyika kesho saa 3 usiku Rabat nchini Morocco.
Advertisement
Back to homepage
Share this story