Banda aliumia bega na kushindwa kuendelea mchezo huo ambao tuliibuka na ushindi wa bao moja katika Uwanja wa Amaan Jumapili iliyopita.
Jopo la madaktari wa klabu limethibitisha Banda atakuwa nje kwa muda huo ambapo ataukosa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Dodoma Jiji utakaopigwa Oktoba 2, katika dimba la Benjamini Mkapa.
Advertisement
Wachezaji wengine wanaoendelea na matibabu ni Pape Sakho aliyeumia kifundo cha mguu na Shomari Kapombe aliyechanika nyama za paja ambao wawili hao hawakusafiri na timu kwenda Zanzibar kwa ajili ya kambi ya wiki moja sanjari ya kucheza mechi mbili za kirafiki.