Simba Sports Club
News

Banda nje miezi mitatu

14 Nov 2022

Banda amefanyiwa vipimo na madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Ibrahim Hajji iliyopo jijini Dar es Salaam na imegundulika amevimba kifundo cha mguu na matibabu yake yatachukua miezi mitatu lakini hatafanyiwa upasuaji.

Banda alipata maumivu katika mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Singida Big Stars uliopigwa Uwanja wa Liti mkoani Singida Novemba 9, huku ambapo alitufungia bao letu la pekee katika mchezo huo.

Advertisement

Awali ilionekana Banda angekaa nje ya uwanja kwa wiki tatu au nne kutibu jeraha alilopata lakini baada ya vipimo vya leo kutoka kwa madaktari bingwa imeonekana atakuwa nje kwa muda mrefu zaidi.

Banda anaungana na nyota wengine wawili Jimmyson Mwanuke na Israel Patrick ambao bado ni majeruhi na wanaendelea na matibabu.

Back to homepage
Share this story