Simba Sports Club
News

Banda: Nimepata uzoefu mkubwa AFCON

5 Feb 2022

Banda raia wa Malawi amesema ni ndoto kwa kila mchezaji kuiwakilisha nchi yake kwenye michuano mikubwa barani Afrika na mara zote ikimalizika unakuwa umejifunza kitu kikubwa.

Banda ameongeza kuwa uzoefu alioupata AFCON atautumia kuisaidia timu yetu kufanya vizuri kwenye mechi yoyote ambayo atapata nafasi ya kucheza.

"AFCON ni michuano mikubwa na kila mchezaji anatamani kushiriki. Kitendo cha kuwa katika kikosi cha nchi yako unajifunza mambo mengi ambayo yanakusaidia kwa sababu unakutana na wachezaji wakubwa Afrika.

Advertisement

"Naamini uzoefu niliopata kwenye mashindano hayo utanifanya kuisaidia timu yangu ya Simba kufanya vizuri," amesema Banda.

Banda amerejea nchini Jumatano kutoka Malawi baada ya kutolewa na Morocco katika hatua ya 16 bora na tayari amejiunga na kikosi kujiandaa na mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya Kwanza.

Back to homepage
Share this story