Simba Sports Club
News

Baleke ni Mnyama

15 Jan 2023 By simbasc 694 views
Uongozi wa Klabu ya Simba unatangaza kukamilisha usajili mshambuliaji wa kati Jean Othos Baleke raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia Congo kwa mkataba wa miaka miwili kutoka TP Mazembe. Baleke (21) anatarajia kuwasili nchini Jumanne na atajiunga na kikosi ambacho kitakuwa kimerejea kutokea Dubai. Baleke amejiunga nasi akitokea Nejmeh FC ya Lebanon ambapo alipelekwa kwa mkopo mwanzoni mwa msimu huu. Usajili wa Baleke ni matakwa ya benchi la ufundi ili kuongeza nguvu kwenye eneo la ushambuliaji. Baleke ni mchezaji wa tatu kusajiliwa kwenye dirisha hili akitanguliwa na Saido Ntibanzokiza na Ismael Sawadogo tuliyemtambulisha jana. Kwa mujibu wa taratibu Baleke ataitumikia Simba kwenye mashindano yote ikiwemo Ligi ya mabingwa Afrika kwani hakucheza katika hatua za awali. Wasifu wa mchezaji Jina Kamili: Jean Toria Baleke Othos Tarehe ya Kuzaliwa: Aprili 17, 2001 Umri: Miaka 21 Urefu: Mita 1,69 Uraia: DR Congo Nafasi: Mshambuliaji wa kati Klabu: Simba.
Advertisement
Back to homepage
Share this story