Nyota hao ni mshambuliaji Jean Baleke kiungo mshambuliaji Kibu Denis na mlinda mlango Ally Salim.
Katika mwezi Aprili tumecheza mechi tano huku nyota hao wakionyesha kiwango bora na kuwa na takwimu nzuri.
Hizi hapa takwimu zao za Aprili
Dakika Mabao Assist
Baleke 407 6 0
Advertisement
Kibu 450 1 3
Ally Salim amecheza mechi nne sawa na dakika 360 akifanikiwa kupata Clean Sheet tatu.
Zoezi la kupiga kura litaanza leo kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz na litafungwa Mei 2 saa sita usiku.
Mshindi atakabidhiwa fedha taslimu Sh 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile.