Simba Sports Club
News

Baleke hajapata majeraha makubwa, kuivaa Coastal Ijumaa

7 Jun 2023

Baleke ameshindwa kuendelea na mchezo wa jana wa ligi dhidi ya Polisi Tanzania na kutolewa dakika ya 13 baada ya kuumizwa na kiungo Salim Ally 'Kipemba'.

Dk. Kagabo amesema Baleke amepata maumivu ya kawaida ambayo hayamfanyi kuwa nje ya uwanja hivyo atafanya mazoezi pamoja na wenzake kesho kujiandaa na mechi ijayo.

Advertisement

"Belake hajapata madhara makubwa katika maumivu aliyopata jana, ilibidi tumpumzishe ili kumkinga asipate madhara makubwa.

"Kesho atafanya mazoezi na wenzake kujiandaa na mchezo dhidi ya Coastal na benchi la ufundi likiona inafaa atakuwa sehemu ya kikosi Ijumaa," amesema Dk. Kagabo.

Back to homepage
Share this story