Baleke amesema anapenda kuona mashabiki wa Simba wakifurahi na yeye pamoja na wachezaji wenzake wapo tayari kuhakikisha hilo linafanikiwa.
Baleke ameongeza kuwa kufanya vizuri kwenye michuano hii mikubwa barani Afrika ni jambo zuri kwakuwa inafungua milango mingine ya mafanikio.
Advertisement
"Natamani sana nifunge, napenda kuona mashabiki wa Simba wakiwa na furaha kwani sisi wachezaji kazi yetu ni kuhakikisha tunawapa furaha.
"Nataka kutengeneza njia nzuri ili kusonga mbele zaidi ya hapa Tanzania, hivyo naomba Mungu aniwezeshe niipiganie timu iweze kushinda," amesema Baleke.