Simba Sports Club
News

Bajaber atupia tukiichapa Mbeya City Meja Isamuhyo

4 Dec 2025

Bajaber alifunga bao hilo dakika ya 87 ukiwa ndio mpira wake wa kwanza baada ya kupokea pasi kutoka Steven Mukwala.

Mshambuliaji wa City, Vitalis Mayanga alitolewa kwa kuonyesha kadi nyekundu dakika ya 23 baada ya kumpiga kiwiko mlinzi wa kushoto, Anthony Mligo.

Morice Abraham alitupatia bao la kwanza dakika ya 27 baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Elie Mpanzu.

Jonathan alitupatia bao la pili dakika ya 37 baada ya mlinzi wa City kukosea kutoa pasi kabla ya mshambuliaji huyo raia wa Ghana kuuwahi na kupiga shuti lililomshinda mlinda mlango Beno Kakolanya.

Kipindi cha pili tulirudi kwa kasi na kufanya mashambulizi mengi langoni mwa City huku mlinda mlango Beno Kakolanya akifanya kazi kubwa ya kuchomoa michomo.

Advertisement

Ushindi huu unatufanya kufikisha alama 12 baada ya kucheza mechi nne tukiwa hatujapoteza mchezo wowote.

X1: Yakoub, Kapombe (Duchu 60') Mligo, Nangu, Chamou, Kagoma, Morice, Kante (Kibu 78') Sowah (Mukwala 60'), Ahoua (Maema 60'), Mpanzu (Bajaber 86')

Waliionyeshwa kadi: Sowah 10'

X1: Kakolanya, Maranyingi, Pillar, Mwaipola (Mwasa 53') Pemba, Stewart, Ambokile (Thobias 66'), Chibada, Matheo (Mwangosi 53'), Mayanga, Daniel

Waliionyeshwa kadi: Mayanga (Nyekundu 23'), Mwasa 68'

Back to homepage
Share this story