Simba Sports Club
News

Babacar Sarr ni Mnyama

6 Jan 2024

Sarr ni kiungo mwenye uzoefu wa kucheza soka la Afrika ambapo mbali na Monastir amewahi kuzichezea Olympique Beja ya Tunisia, Teungueth FC, AS Pikine na Mbour P.C.

Sarr ana uwezo mkubwa wa kucheza kama kiungo mkabaji na wakati mwingine anaweza kucheza kama kiungo mshambuliaji kwahiyo ni jambo ambalo limetuvutia.

Advertisement

Sarr anakuja kuungana na viungo wakati kama Fabrice Ngoma, Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin na Abdallah Khamis.

Sarr anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa katika dirisha hili la usajili baada ya kiungo Salem Karabaka ambaye tumemsajili kutoka JKU ya Zanzibar mwanzoni mwa wiki hii.

Back to homepage
Share this story