Simba Sports Club
News

Babacar aanza mazoezi Zanzibar

7 Jan 2024 By simbasc 438 views
Kiungo mpya mkabaji, Babacar Sarr ameanza mazoezi ya utimamu wa mwili ili kujiweka sawa kabla ya kujiunga moja kwa moja na wenzake. Babacar amekamilisha usajili wake jana na tayari yupo Zanzibar na kikosi huku akifanya mazoezi chini ya uangalizi wa kocha wa viungo. Babacar amekuja Zanzibar na kuanza mazoezi moja kwa moja ili kuweza kuwazoea mapema wenzake pamoja na mazingira ili atakpoanza kupata nafasi isiwe changamoto kwake. Kama utimamu wake utakuwa vizuri tunaweza kumuona Babacar katika michezo ya mwishoni ya michuano hii ya Mapinduzi kwa vile ambavyo kocha Abdelhak Benchikha ataona inafaa.
Advertisement
Back to homepage
Share this story