Simba Sports Club
News

Baba mzazi wa Chama aitembelea Simba Zambia

5 Dec 2021

Baba mzazi wa kiungo wetu wa zamani Clatous Chama, mzee Clatous Chama Senior leo amekitembelea kikosi chetu kambini kwa ajili ya kusalimia na kukipa hamasa kabla ya kwenda uwanjani kushuhudia tukicheza na Red Arrows.

Mzee Chama alikuja kwenye hoteli tuliyofikia na kukutana Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez na Wajumbe wa Bodi waliombatana na timu kuzungumza mambo kadhaa.

Advertisement

Mzee Chama alikuja kututakia heri kwa ajili ya kufuzu michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na jambo la kushukuru ni kuwa tumefanikiwa.

Chama ni mmoja ya wachezaji wenye majina makubwa nchini Zambia ambapo mafanikio makubwa ameyapata akiwa nasi kitu ambacho kimemvutia baba yake kuja kutuona.

Back to homepage
Share this story