Baada ya kutupia bao moja lilohitimisha ushindi wetu wa mabao 3-1 dhidi ya Ruvu Shoouting jana, Mshambuliaji Kibu Denis amesema anategemea kuendelea kufunga na kuisaidia timu kupata pointi tatu kila mechi.
Kibu amesema ni furaha kwake kufungua akaunti ya mabao ambayo anaamini imemuongezea hali ya kujiamini na kujituma ili kuhakikisha timu inapata matokeo.
Nyota huyo amewaomba mashabiki wetu kuendelea kuwapa sapoti wachezaji kwani nyakati za furaha zinarejea ndani ya kikosi chetu.
"Ni furaha kufunga bao langu la kwanza nikiwa Simba, limeongeza hali ya kujiamini na kujituma zaidi ili niendelee kufunga kila nikipata nafasi.
"Nimecheza mechi tatu mfululizo bila kufunga, nilijipa moyo na kuendelea kujituma na jana nimefanikiwa kufunga na ninaamini nitaendelea kufanya hivyo," amesema Kibu.