Simba Sports Club
News

Awesu yupo huru kuichezea Simba

15 Aug 2024

Baada ya majadadiliano ya pande mbili na KMC tumefikia muafaka kuwa Awesu ni mchezaji wetu halali na tutakuwa nae kwa muda wa miaka miwili kwa mujibu wa mkataba aliyosaini.

Awesu ni mmoja ya wachezaji wenye kipaji kikubwa ndio maana Uongozi wa klabu umehakikisha unamaliza suala hili ili aweze kuwa sehemu ya kikosi chetu kwa ajili ya msimu wa mashindano 2024/25.

Advertisement

Hivi sasa Awesu yupo kambini na timu inayojiandaa na mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Tabora United utakaopigwa Agosti 18 katika Uwanja wa KMC.

Back to homepage
Share this story