Simba Sports Club
News

Aubin Kramo ni Mnyama

7 Jul 2023

Kramo (27) raia wa Ivory Coast ni mchezaji mwenye uzoefu kwenye michuano ya Afrika ambaye tunaamini atakuwa msaada mkubwa kwenye kikosi kuelekea msimu mpya wa Ligi 2023/24.

Kramo ambaye anatumia mguu wa kushoto ana uwezo wa kucheza nafasi mbalimbali uwanjani kama winga zote mbili na kucheza nyuma ya mshambuliaji kama namba 10.

Katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita, Kramo amefunga mabao manne katika mechi 10 alizocheza akiisaidia ASEC kufika Nusu Fainali.

Advertisement

Kramo ameiwezesha ASEC kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu nchini Ivory Coast (MTN Ligue 1).

Kramo anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa kuekea msimu mpya wa ligi baada ya Leandre Willy Onana raia wa Cameroon tuliyemtangaza juzi Jumanne.

Back to homepage
Share this story