Simba Sports Club
News

Asante Israel Mwenda

13 Aug 2024

Israel alisaini mkataba mpya wa miaka miwili kuitumikia Simba, lakini kabla ya kuanza kutumikia mkataba huo aliandika barua ya kuomba kuondoka kwa madai amepata klabu sehemu nyingine.

Simba kwa kujali na kuheshimu mahitaji ya wachezaji wetu alipewa masharti ya kurejesha fedha zote za usajili na tayari amesharejesha na sasa yupo huru kujiunga na timu yoyote.

Advertisement

Simba inathamini mchango wa Israel katika miaka yote mitatu aliyodumu nasi, tayari nafasi ya Israel Mwenda imeshazibwa na Kelvin Kijili.

Uongozi wa klabu unamtakia kila la heri Israel katika maisha yake mapya ya soka.

Back to homepage
Share this story