Ahoua alijiunga na kikosi chetu Julai, 2024 kutoka Stella Club Abidjan ya Ivory Coast akiwa mchezaji bora wa msimu wa Ligi hiyo (MVP).
Katika msimu wake wa kwanza akiwa na kikosi chetu Ahoua ameibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu ya NBC akiwa amefunga mabao 17.
Katika kipindi cha mwaka mmoja na nusu alichodumu ndani ya Simba, Ahoua amekuwa mchezaji muhimu wa makocha wote waliopita kikosini kwetu.
Advertisement
Moja ya kumbukumbu nzuri atakazo kumbukwa Ahoua ni uwezo mkubwa wa kufunga na kutengeneza nafasi kupitia mipira ya adhabu nje ya 18.
Uongozi wa klabu unamtakia kheri Ahoua katika maisha yake mapya ya soka nje ya Simba.