Ally ambaye ameonyesha uwezo mkubwa kwenye mechi zetu zilizopita amewapiku kiungo mshambuliaji Kibu Denis na mshambuliaji Jean Baleke aliokuwa anawania nao tuzo hiyo.
Katika mwezi Aprili, Ally amecheza mechi nne sawa na dakika 270 akiondoka na 'clean sheet' tatu akiruhusu bao moja.
Mchanguo wa kura zilivyopigwa
Kura Asilimia
Baleke 414 22.84
Advertisement
Kibu 655 36.13
Ally 744 41.04
Ally anakuwa mlinda mlango wa kwanza kushinda tuzo hiyo tangu ilivyoanza kutolewa miaka miwili iliyopita.
Ally atakabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile ikiwa ni zawadi ya kuibuka mshindi wa kinyang'anyiro hicho.