Simba Sports Club
News

Alichosema Seleman Haroub kwenye Uzinduzi wa Wiki ya Simba

30 Aug 2025

Haroub amesema mpangilio wa Simba Day ni wa tofauti na kikosi chetu cha msimu huu ni imara zaidi huku pia burudani ikiwa ni ya kutosha.

Bw. Haroub ameongeza kuwa hata mapokezi tuliyopata kwenye uzinduzi wa wiki ya Simba uliofaanyika Uwanja wa Wambi, Mafinga mkoani Iringa unaonyesha kuwa Simba Day ya mwaka huu haitakuwa ya kawaida.

"Uzinduzi mkubwa kama huu ni ishara kubwa kuelekea msimu mkubwa na usajili wenyewe si mmeona, siku ya kuona zaidi ni Simba Day wote tuliopo hapa tuhakikishe tunafika uwanja wa Mkapa, Kuna vitu hamjawahi kuona vikitokea mwaka huu mtaona," amesema Haroub.

Advertisement

Kuhusu kikosi Bw. Haroub amesema msimu uliopita kocha Mkuu Fadlu Davids na benchi lake la ufundi ilianzisha project lakini sasa imekomaa na inakwenda kufanya kazi.

"Ile project ya Kocha Fadlu ambayo alianzisha mwaka jana mwaka huu ndio inakwenda kufanya kazi vizuri. Tuendelee kuwapa ushirikiano viongozi wetu tukianzia na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Bilionea, Mohamed Dewji 'Mo' na Mwenyekiti wa Klabu, Murtza Mangungu,"

Aidha Bw. Haroub amedokeza kuhusu Uzinduzi wa jezi zetu za msimu ambapo amesema "Kesho tunafanya uzinduzi wa jezi pale Super Dome Masaki kila Mwanasimba ahakikishe ananunua jezi yake mapema. Jezi zetu ni nzuri hivyo napenda kuwasihi mhakikishe mnanunua ili tupendeze siku ya Simba Day."

Back to homepage
Share this story