Simba Sports Club
News

Alichosema Robertinho kuhusu mchezo na African Sports Kesho

1 Mar 2023

Robertinho amesema siku zote malengo ya Simba ni kushinda kila taji la michuano tunayoshiriki kwa hiyo tunahitaji kupata ushindi kesho.

Amesema kesho anategemea kuwatumia wachezaji ambao hawapati nafasi kubwa kikosini kwa kuwa wiki ijayo tuna mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vipers.

Advertisement

"Tumejipanga kuhakikisha tunashinda mchezo wa kesho wa ASFC dhidi ya African Sports, Simba ni timu kubwa na tunahitaji kushinda kila taji na tupo tayari.

"Tunategemea kuwatumia wachezaji ambao hawajapata nafasi kubwa kikosini kwa kuwa tuna mchezo wa marudiano nyumbani dhidi ya Vipers kwa hiyo tunaziangalia mechi zote," amesema Robertinho.

Back to homepage
Share this story