Robertinho amesema amepata nafasi ya kuwatazama Ihefu na kugundua wanacheza kitimu na wakati mwingine wanatumia nguvu kwahiyo tumejipanga kuhakikisha tunawakabili.
Robertinho amebainisha kuwa Simba ni timu kubwa na anawaamini wachezaji wetu hivyo tutapambana kuhakikisha tunapata ushindi.
"Siku mbili nyuma nimewatazama wapinzani wetu wanacheza vizuri lakini Simba ni kubwa na tunaamini tutacheza soka safi na kupata ushindi," amesema Robertinho.
Kwa niaba ya wachezaji mshambuliaji, Shabani Chilunda amesema kwenye ligi kila mechi ni ngumu ila wao wamejiandaa kuhakikisha tunacheza soka safi na kushinda.
"Mechi itakuwa ngumu, tunaiheshimu Ihefu lakini tumejiandaa vizuri. Kila mchezaji atayepata nafasi atakuwa tayari kuipigania timu kupata ushindi," amesema Chilunda.